Duration 1:13

KARIA APELEKWA MAHAKAMANI/UCHAGUZI KUZUILIWA

1 005 watched
0
2
Published 1 Jul 2021

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepokea kesi ya kupinga uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyofunguliwa na Ally Saleh 'Alberto' ambaye alikuwa moja ya wagombea kwenye uchaguzi huo. Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 8 Agosti, 2021, jijini Tanga, ambapo mpaka sasa kamati ya uchaguzi imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Urais. Kesi hiyo ya madai namba 98 ya mwaka 2021, iliyofunguliwa na Ally Salehe, raia wa Tanzania anayeishi Zanzibar ambayo itakuwa chini ya Jaji Kakolaki ambapo wadai ni TFF, Bodi ya wadhamini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba. Mahakama hiyo pia imewataka wadaiwa hao wote watatu kufika kesho mahakamani hapo, kujibu hoja ya kwanini uchaguzi huo usisimamishwe. 🔘JE, NA WEWE UNA HABARI? 🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402), 🔘WhatsApp ( +255 692 318213) 🔘Email: mwanahalisitvnews@gmail.com 🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com

Category

Show more

Comments - 0