Duration 1:41

JITIHADA NI MAFANIKIO | Hamasa Ep. 37

5 929 watched
0
118
Published 22 Jul 2020

JITIHADA NI MAFANIKIO | Hamasa Ep. 37 Kila hatua ni matokeo ya hatua na hakuna hatua ambayo chanzo chake sio hatua. Hatua unayoinua sasa haiwezi kuwa bure, isipokuwa ina matokeo ambayo kesho yatadhihirika, hata kama itakuwa hatua yenye udogo kiasi gani. Binadamu ni viumbe wa matokeo kwahiyo usitarajie sana kuungwa mkono kwenye hatua zako, simama mwenyewe kwani hata mafanikio unayotafuta yatakuwa ni yako na si yao. Mwanzo wa kikubwa huwa ni kidogo na hakuna aliyefika kumi bila kupita moja, na hiyo ndio kanuni mama ya mafanikio. Maisha unayoishi leo ni msingi mzuri wa kesho yako. kuchekwa au kebehi za walimwengu zisikurudishe nyuma, endelea kupambana kwenye kutimiza ndoto zako. Boresha tabia zako ziwe za mafanikio kwani kamwe hakuna mafanikio yanayogonga mlango wa mtu ni lazima yatafutwe kwa bidii na utaratibu maalum. Haijalishi kipato chako, kikubwa au kidogo jifunze nidhamu ya fedha. Kuwa na matumizi yanayoendana au kuwiana na kiasi gani cha pesa umeingiza. Hatua zako ni mafanikio yako. Piga hatua sahihi leo hii Imeandikwa na: Abdulrazaki Issa. . Usiache ku SUBSCRIBE na kuniachia mawazo yako kwenye COMMENTS, LIKE na SHARE PIA kwa wengine. . NIFUATE MITANDAONI INSTAGRAM: https://www.instagram.com/ezdenjumanne/ TWITTER: https://www.twitter.com/ezdenjumanne FACEBOOK: https://www.facebook.com/ezdenjumanne LINKEDIN: https://www.linkedin.com/in/ezdenjumanne . BIASHARA NA MATANGAZO: EMAIL: successpathnetwork@gmail.com PHONE: A text | Whatsapp : (+255)759191076 #Jitihada #Mafanikio #Hamasa

Category

Show more

Comments - 14