Duration 2:42

MANENO YA KWANZA YA MDUDE NYAGALI BAADA YA KUACHIWA HURU NA MAHAKAMA.

410 watched
0
4
Published 28 Jun 2021

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeimemuachia huru Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mdude Nyagali Katika kesi iliyo kua inamkabili kesi namba 36 ya Mwaka 2020 ya kusafirisha dawa za kulevya. Akisoma hukumu hiyo iliyo chukua taklibani dakika thelathini Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Zawadi Leiser amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha pasina shaka kuwa mshitakiwa mdude nyagali alitenda kosa hilo. Hakimu huyo Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Zawadi leizer amesema wamepitia kwakina ushaidi wa pande zote mbili wakati upande wa mashitaka ulikua na mashahidi nane wakiwa na vilelezo 14 huku upande wa utetezi ulikua na shahidi mmoja na vielelezo vitatu. Hakimu zawadi amesema katika kesi hiyo upande wa mashitaka uliwasilisha vielelzo 14 ikiwemo dawa za kulevya ambazo zilipatikana nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya upekuzi uliofanywa nyumbani kwake. Amesema upande wa utetezi ukaieleza mahakama kuwa kabla ya upekuzi huo mshitakiwa alipo kamatwa funguo za nyumbani kwake pamoja na simu zilichukuliwa na jeshi la polisi na kuibua shaka kuhusu upekuzi uliofanywa na jeshi hilo kitu ambacho kilikua ni kinyume na sheria namba 20 mapitio ya mwaka 2019 kifungu cha 38 kifungu kidogo cha 2 na kifungu namba 42. Amesema baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili mahakama imebaini kwam,ba upekuzi ulio fanywa nyumbani kwa mtuhumiwa ulikua ni batili kwakua hakukuwepo kwa kibali cha upekuzi,funguo za mtuhumiwa kushikiliwa na polisi tangu alipo kamatwa pamoja na mmoja wa wapekuzi kutoka nje wakati wa zoezi hilo huku mtuhumiwa akiwa chumbani. Baada ya mahakama hiyo ya hakimu mkazi mkoa wa mbeya kumuachia huru kada huyo wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mdude nyagali amesema anaipongeza mahakama kwa kumtendea haki katika kesi hiyo huku akielezea iwe niendelevu wa kutenda haki. ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA BIG STAR TV ( +255 623 715536), ( +255 718 613054) ⚫️ Email: info@bigstarfm.co.tz ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ THE KICK NA ADVERA MABIKI : ⚫️ Subscribe Big Star TV

Category

Show more

Tags

Comments - 1