Duration 7:37

DINI YA AJABU YAIBUKA DAR, WAUMUNI WAKE HAWAAMINI KIFO

313 461 watched
0
1.1 K
Published 3 Aug 2019

DINI YA AJABU YAIBUKA DAR, WAUMUNI WAKE HAWAAMINI KIFO! DUNIA ina mambo! Ukiambiwa kuna imani ya dini inayofundisha waumini wake kwa kutumia vitabu viwili vitakatifu vya Biblia na Quran kwa wakati mmoja, utashangaa. Hiyo ndiyo dini ya ajabu iliyoibuka Bongo, ambapo kiongozi wake, aliyejitambulisha kwa majina mawili – Nabii Eliya au Nabii Ilyaas anatoa huduma hiyo maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani. Gazeti hili linamuibua nabii huyo, ikiwa ni siku chache tangu mtu mmoja, aitwaye Michael Job ambaye hujiita Yesu, alipokamatwa nchini Kenya na kurudishwa kwao Marekani. Ilielezwa kuwa, jamaa huyo alialikwa nchini Kenya na mchungaji mmoja ambaye hakutajwa jina wala kanisa lake, ambapo alikuwa akipita mitaani na kuwaaminisha watu kuwa yeye ni Yesu Kristo na angewapeleka mbinguni. Job ambaye ni mwigizaji wa Hollywood, nchini Marekani alikuwa akipita mitaani huko Kenya na kukusanya fedha kama sadaka kabla ya kudakwa na kurudishwa kwao hivi karibuni, lakini mchungaji aliyemwalika akatiwa nguvuni. DINI YA AJABU BONGO Risasi Jumamosi lilipokea malalamiko kutoka kwa chanzo chetu, ambacho kilipiga simu katika chumba cha habari cha gazeti hili, kikieleza kuwepo kwa dini hiyo, maeneo ya Misugusugu Karabaka na kuwapa usumbufu mkubwa raia. “Jamani huku Misugusugu sisi wananchi wa hapa Misugusugu Karabaka, kuna nabii ambaye hatumuelewi. Amefungua sijui ni msikiti, sijui ni kanisa na anafundisha watu kwa kutumia Biblia na Quran kwa wakati mmoja. “Waumini wake wanavaa kanzu kama Waislam, lakini mambo yao ndiyo yanayotukera. Maombi wanayofanya hatujui ni ya aina gani, maana wanaimba usiku kucha. “Kuna wakati utawasikia wanaimba kama Waislam, wakati mwingine kama Wakristo kwa kiswahili cha kawaida. “Kuna wakati usiku huwa wanakimbiakimbia kama wanafanya mazoezi. Sisi majirani hatuwaelewi wako upande gani na wala hatujui huwa wanakula muda gani maana wapo bize muda wote,” kilieza chanzo hicho. MGONJWA AFARIKI WAKIMUOMBEA Kikiendelea kutiririka chanzo hicho kinasema kuwa, kuna wakati mgonjwa alipelekwa kwa Nabii Eliya kuombewa, akafariki dunia kisha wakaanza kumuombea afufuke bila mafanikio. “Huyo mgonjwa alikuwa mwanamke, anaitwa mama Halima. Alipelekwa na mume wake. Wote ni waumini wake, lakini katikati ya maombi, huyo mama akafariki dunia. /playlist?list ... /watch/f-X1N-1 ... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/

Category

Show more

Comments - 1429